Home Uncategorized Sio story mpya Snoop Dogg kukamatwa kisa dawa za kulevya, imemkuta tena...

Sio story mpya Snoop Dogg kukamatwa kisa dawa za kulevya, imemkuta tena Sweden… Kilichofuatia?

SNOOPY

Najua kukutana na story ya Rapper Snoop Dogg kukamatwa na Polisi sio story mpya kabisa, ishu ni kwamba jamaa alienda kwenye show Sweden, baada ya kumaliza akanaswa tena na Polisi wakati akiwa anajiandaa kurudi zake Marekani !!

Snoop alikamatwa akihusishwa na kosa la kutumia dawa za kulevya kitu ambacho ni kinyume cha Sheria za Sweden… baada ya kumfanyia vipimo vya Uchunguzi walimwachia baada ya vipimo kuonesha jamaa hakuwa ametumia dawa hizo.

Kiukweli jamaa alikasirishwa sana na hii ishu na anaona kama Polisi walionesha vitendo vya Kibaguzi kumkamata, baada ya hapo jamaa kaapa kwamba hatamani hata kidogo kurudi tena Sweden >>>> “Samahani sana mashabiki wangu wote wa Sweden, sitorudi tena kwenye nchi hii… Mtamshukuru Bosi wenu wa Polisi na wahusika wote wa Idara ya Polisi ila ndio nshamaliza” >>>> Snoop Dogg.